Vibrant

Friday, 4 April 2014

TUME YAANZA UTAFITI KATIKA MAPITIO YA MFUMO WA SHERIA UNAOSIMAMIA HAKI ZA WALAJI

Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Adam Mambi akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa kuanza utafiti katika mapitio ya mfumo wa sheria unaosimamia haki za walaji ikiwa ni hatua mojawapo katika mchakato wa kuundaa  sheria inayowalinda watumiaji wa huduma mbalimbali hapa nchini. Kulia ni Afisa Sheria wa Tume hiyo ni Fred Kandonga.

Afisa Sheria wa wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Fred Kandonga akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu sababu zilizopelekea Serikali kuamua kufanya utafiti utakaopelekea kutungwa kwa sheria itakayosaidia kuwepo kwa mfumo nwa biashara wenye uwiano katika ushindani. Katikati ni Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Adam Mambi, anayemfuatia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi na Mwisho kushoto ni Afisa habari wa Tume hiyo Munir Shemweta.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA

Anuani ya simu: "TUMESHERIA”.                                                                                P.O.Box 3580      
Simu ya mdomo; 2111387/2123533/4                                                                      DAR ES SALAAM
Namba ya fax: 2123534                                                                                                                                              
Barua pepe: lrct@lrct.go.tz
                                                                  
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TUME YAANZA UTAFITI KATIKA MAPITIO YA MFUMO WA SHERIA UNAOSIMAMIA HAKI ZA WALAJI

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeanza kufanya utafiti wa  mfumo wa sheria unaosimamia Haki  za Walaji ili kubaini kasoro mbalimbali zilizoko kwenye  mfumo husika na kupendekeza njia sahihi ya kuboresha mfumo huo nchini Tanzania.

Hatua ya Tume kufanya utafiti huo inatokana na mendeleo ya sayansi, teknolojia pamoja na utandawazi ambayo kwa ujumla yamemfanya mlaji kujikuta akiwa kwenye hatari ya kuathirika kiafya, kiuchumi na kijamii.

Tume katika utafiti wa awali, imebaini kuwa Mfumo uliopo hauendani na  na wakati huu wa mabadiliko ya kiuchumi, kijsamii, kitekenologia yanayotokea, kwani sheria nyingi zilizopo zilitungwa muda mrefu na hivyo hazikuzingatia mahitaji ya wakati wa sasa.

Pia sheria nyingi  hazijajumuishwa kwenye sheria moja  zinasimamiwa na watu au Taasisi tofauti tofauti. Hivyo, Tume imeona haja ya kupitia sheria hizo ili kupendekeza  mfumo wa sheria utakaomlinda mlaji kwa kuzingatia maendeleo yaliyopo sasa.
Na ni matarajio yetu baada ya kukamilika kwa utafiti huu Tume tutakuja na mapendekezo ambayo yataleta tija kwa walaji wetu pamoja na taifa kwa ujumla.
Tume ya Kurekebisha Sheria (Tume) ilianzishwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Kurekebisha Sheria Namba 11 ya mwaka 1980. Sheria hii kwa sasa ni Sura ya 171 ya Sheria za Tanzania Toleo la Mwaka 2002. Tume ya Kurekebisha Sheria ni Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara ya Katiba  na Sheria. 

Imetolewa na;
Tume ya Kurekebisha Sheria (T)
Dar es Salaam
04 Aprili, 2014


BIG RESULTS NOW' KUFANIKISHA UBIA KATI YA SEKTA BINAFSI NA ZA UMMA

Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, hivi karibuni. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now). Picha na Sufianimafoto.com