Wednesday, 26 March 2014
WAJUMBE BUNGE LA KATIBA WATAKIWA KUZINGATIA MASLAHI YA TAIFA
Na Magreth Kinabo – Maelezo, Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Maalum la Katiba wamewataka wajumbe wenzao kujitika katika mchakato wa mjadala wa Rasimu ya Katiba Mpya itakayozingatia maslahi ya taifa na kuwanufaisha Watanzania badala kujitazama mwenyewe.
Kauli hiyo imetolewa leo na mjumbe wa bunge hilo, ambaye ni mmoja wa kiongozi wa kundi la TANZANIA KWANZA Dk. Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Tanzania(TBC), ambapo alisema msingi wa kundi hilo ni kushiriki katika mchakato huo na kuaichaTanzania ikiwa moja.
“ Tunataka kushiriki katika kumaliza kazi ya Bunge hili na kuaicha Tanzania ya leo na Kesho baada kumaliza ,” alisema Dk. Nchimbi.
Aidha DK . Nchimbi alisema kuwa mchakato huo usiwe sehemu ya kujipatia madaraka, bali iwe ya kuwaongoza Watanzania katika kuwapatia maendeleo.
Alisema bado watu wana mahitaji makubwa ya huduma za kijamii kama vile elimu, afya, ufugaji, na miundombinu.
Dk. Nchimbi akifafanua kuhusu suala la kura ya wazi au siri, alisema bado msimamo wake ni wa kura ya wazi ambao utajenga mfumo wa maadili ya ukweli na uwazi, huku akihoji kama wanachangia mjadala kwa wazi kwa nini kura zisipigwe kwa wazi?
Alisema kura ya wazi itasaidia wananchi kutambua michango yao katika maeneo mbalimbali ilivyowakilishwa.
“Tuko hapa kutunga Katiba ya Watanzania mtu atakumbukwa kwa kile alichokisema,” alisisitiza.
Kwa upande wake mjumbe mwingine wa kundi hilo , Charles Mwijage akingumza katika kipindi hicho aliwataka wajumbe wa Bunge hilo kutumia njia ya maridhiano pale wanapoona kuna mambo ambayo hajaridhika nayo.
Akizungumzia kuhusu suala la kuwepo kwa Serikali tatu alisema , lina gharama ya kuuendeshaji kwani ,italazimika kuwa na tume nane kuwa na mabunge matatu yenye viongozi tofauti ambayo yataongeza gharama
Akizungumza baada ya kuahirishwa wa kikao cha Bunge hilo, mjumbe kutoka Asasi ya Vijana, Siti Abbas Ali , ambaye pia ni Mwanasheria kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) aliwataka Watanzania kuondoa hofu juu ya mchakato huo,hivyo katiba hiyo itakuwa ni ya Watanzania.
Alisema wataangalia kwa upana haki za vijana, watoto, wanawake na makundi maalum kwa upana. Mwisho.
TAMKO RASMI LA MTANDAO WA WATU WA PEMBA WAISHIO TANZANIA BARA
NEPPELTA
NETWORK FOR
PEOPLE OF PEMBA LIVING IN TANZANIA MAINLAND
MTANDAO WA
WATU WA PEMBA WAISHIO TANZANIA BARA
MAKUNGANYA STREET/ KARIAKOO
P.O. BOX 21243
DAR
ES SALAAM
23/03/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI.
TAMKO RASMI LA KUUNGA MKONO
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE
LIYOITOA KWA BUNGE MAALUMU LA KATIBA, DODOMA TAREHE 21/03/2014.
Ndugu,
Waandishi wa habari, Tunamtanguliza
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehemu, heri na Baraka.
Mpango
wa kuunganisha nchi za Zanzibar na Tanganyika ambao mchakato wake ulianza mwaka
1963 ulikuwa ni utashi wa Viongozi wetu wawili Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Marehemu Mzee Abeid Aman Karume.
Wote
wawili kupitia vikao vyao mbalimbali walikubaliana kuziunganisha nchi hizi kwa
maslahi mema ya wananchi wao. Hatua hiyo ilipewa Baraka na Mabunge ya nchi hizi
mbili na miswada ya sheria ya kuunganishwa ilipitishwa na ikatungwa sheria
iliyopelekea kufanyika tendo la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 24
Aprili 1964.
Dhima
ya Muungano wetu pamoja na mambo mengine ni kuimarisha historia ya vizazi vya
nchi hizi mbili ambazo zina asili zinazofanana na historia za asili hizi
zilivurugwa na Wakoloni wa Kijerumani, Kiingereza na hatimaye utawala wa
Sultan.
Tangu
Muungano ufanyike kumekuwa na mabadiliko mbalimbali hasa katika mahusiani ya
kibiashara.
Sisi
Watanzania wenye asili ya Pemba tunaoishi huku Bara tumefaidika na tunaendelea
kufaidika sana na uwepo wa Muungano. Ukiachilia suala la ajira za Serikalini,
Muungano umesaidia kukua kwa biashara zetu ambapo mtaji wa Wapemba pekee
wanaoishi huku umeweza kufikia shilingi Trilioni 1.2. Hiki si kiasi kidogo kwa
nchi kama Tanzania inayopigania ukuaji wa uchumi kupitia mitaji ya uwekezaji
hasa wa kizalendo.
Idadi
ya Wapemba wanaoishi Bara imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo hadi
mwaka 2012 inakadiriwa kwa kufikia laki 8.3. Faida nyingine pia ni sisi kuoa au
kuolewa na wenzetu wa Bara hali iliyochangia kuongezeka kwa mahusiano ya
kindugu. Pia Wapemba wamejihusisha zaidi na Kilimo na ufugaji na kuongeza tija
zaidi katika sekta hizo.
Hivyo
basi kuwepo kwa dalili zozote za kuvunjika kwa Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar hakuwezi kutuacha salama sisi Wapemba tuishio huku Bara. Chokochoko
zote na ishara mbaya za chuki kati ya Wabara na Wazanzibar hazitaweza
kuimalisha msingi mkubwa wa Muungano uliojengwa kwa muda mrefu chimbuko lake
likiwa ni waasisi wetu.
Kwa
hatua hiyo basi mtandao wetu umeona si vyema kukaa kimya bila kumpongeza Rais
wetu Dk. Jakaya Kikwete kwa hotuba nzuri iliyojaa hekima, busara, uzalendo na
upole. Sisi tumefarijika sana Rais wetu kukemea Serikali tatu kwa kuonyesha
udhaifu wa kila mmoja huku akijenga hoja zenye mshiko kuhusu athari za Serikali
hizo kwa uwepo wa Muungano huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)