Vibrant

Thursday 13 March 2014

Tunajivunia Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar


Samia Suluhu arudisha Fomu ya kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bunge Maalum la Katiba


Kina Mama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimsindikiza Mjumbe wa Bunge Hilo na Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan(Aliyenyanyua fomu)kurudisha fomu kwa Katibu wa Bunge Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila akitoa maelekezo kwa wapambe wa mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya kupokea Fomu hizo Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu akizipitia Fomu kabla ya Kuzikabidhi kwa Katibu wa Bunge tayari kwa uchaguzi utakaofanyika jioni ya leo Mjini Dodoma.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila akisaini fomu za mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.

Tanzania Kuwa na Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimweleza Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon, Mipango mbalimbali inayofanywa na Tanzania kuimarisha uhusiano na Korea Ikiwamo ufunguaji wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea, wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon akimweleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda mpango wa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala yatakayochangia maendeleo kwa nchi na wananchi husika.

Wajumbe wa Kamati za Mambo ya Nje za Tanzania na Korea wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimpa zawadi Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon wa Mwisho kulia ni Mkurugenzi Mkazi Ujirani Mwema, leo Mjini Dodoma.