Vibrant

Monday, 14 April 2014

TBS KUINUA WAJASIRIAMALI WADOGO NCHINI

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Vedastina Justinian akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mradi wa Vituo vya Utoaji Huduma kwa Pamoja Mipakani (One Stop Border Posts) unaolenga kurahisisha taratibu za forodha, uhamiaji, usimamizi wa ubora wa bidhaa, ulinzi na usalama. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi Mhandisi Abdillah Mataka na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.

Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi kutoka Wizara ya  Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhandisi Abdillah Mataka, akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo katika kujenga vituo vya utoaji huduma mipakani kwa kila nchi husika ili kurahisisha shughuli za utoaji huduma za forodha na uhamiaji. Ujenzi wa vituo hivyo hapa nchini unafadhiliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo ya Japan. Kushoto ni Mchumi Idara ya Biashara na Sekta za Uzalishaji kutoka wizara hiyo Bw. Amedeus Mzee.

Mchumi Idara ya Biashara na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Amedeus Mzee akizungumzia faida zitakazopatikana kwenye mradi wa vituo vya utoaji huduma kwa pamoja mipakani, aidha alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na watumishi wa vituo hivyo katika kuhakikisha mapato hayapotei kwa maslahi ya nchi yetu na jumuiya kwa ujumla.

SERIKALI KUKAMILISHA VITUO VYA UTOAJI HUDUMA MIPAKANI

WIZARA YA  USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Na Frank Mvungi-Maelezo

Serikali imejipanga kukamilisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja Mipakani (One Stop Border Posts-OSBP) vitakavyosaidia kurahisisha taratibu za forodha,uhamiaji,Usimamizi wa ubora wa bidhaa na huduma ,usalama na ulinzi kwa kutoa huduma hizi upande mmoja wa mpaka.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vedastinian Jastinian wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akieleza faida za vituo hivyo, Vedastinian amesema vitaondoa urasimu uliokuwepo awali na kuharakisha huduma na kwa wananchi wa nchi wanachama wakati wanapotaka kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Alisema Kituo cha kwanza ni kile cha Holili ambacho kimekamilika na kimekabidhiwa  kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao ndio waendeshaji wa vituo hivyo hapa nchini ambapo mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2014.
Alifafanua kuwa katika mipaka ya Sirari/Isebania unazitenganisha Tanzania na Kenya na kwa upande wa Mkoa wa Mara mpaka wa Mutukula unazitanganisha Tanzania na Uganda.

Vedastinian alivitaja vituo vingine kuwa ni Namanga cha Arusha,Kabanga/Kobero kilichopo mpakani mwa Tanzania na Burundi unatarajiwa kukamilika mapema mwezi novemba 2014.

Alitaja vituo vingine ni Horohoro Mkoani Tanga na Lungalunga upande wa nchi ya Kenya ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika mapema mwaka huu.
Mradi huo unatekelezwa baada ya kutungwa sheria ya jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuanzisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja mipakani (OSBP) Katika nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sheria iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na Iko katika hatua za mwisho za kuidhinishwa na Wakuu wan chi wanachama.


WATUMISHI WA UMMA WAFANYA BONANZA LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO





Baadhi ya watumishi wa Umma kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali wakifanya mazoezi mepesi wakati wa Bonanza la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano lililofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.