Friday, 25 April 2014
UTUMISHI YAICHAKAZA CDA MASHINDANO YA MEI MOSI
Na.
James Katubuka
Timu ya Mpira wa pete ya
ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeendelea kujiweka katika nafasi
nzuri ya kuwa bingwa wa michuano ya Mei Mosi mwaka huu mara baada ya kuilaza
CDA ya Dodoma magoli 42 dhidi 15 katika mchezo uliofanyika jana Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezo huo ulikuwa na
ushindani wa aina yake kutokana wachezaji wengi wa CDA kuwa ni wazoefu na Ofisi
ya Rais Utumishi kuwa na wachezaji ambao wengi wao wameshaichezea timu ya Taifa
kwa nyakati tofauti.
Licha ya washabiki wa mpira
wa pete mjini Morogoro kushuhudia burudani safi pia walishuhudia jahazi la timu
ya CDA likizama katika kipindi cha kwanza kwa kubugizwa magori 16 dhidi ya matano katika mchezo huo.
Hadi mwamuzi wa mchezo huo
anapuliza kipenga cha mwisho kuashiria mchezo huo kwisha, wachezaji wa Ofisi ya
Rais Utumishi Fatuma Machenga (GA) na Mwadawa Twalibu (GS) walishirikiana vema
kuilaza CDA mabao 42 dhidi ya 15.
Nao wachezaji Anna Msulwa
(WA) na Elizabeth Fusi (C) walikuwa ni chachu ya ushindi kwa timu ya utumishi
kutokana na kuwalisha vema Fatuma Machenga (GA) na Mwadawa Twalibu (GS) katika
mchezo huo uliotawiliwa na ufundi na shamla shamla toka timu pande zote mbili.
Mara baada ya mchezo
kumalizika, kocha wa timu ya CDA Dodoma Bi. Susan Nkurlu alisema kuwa mchezo
ulikuwa mzuri na wa kuvutia hivyo aliwapongeza wachezaji wake na wa Utumishi
kwa kutoa burudani safi kwa wapenzi wa mpira wa pete wa Morogoro.
“Kukosekana kwa kwa wachezaji
wangu nyota wawili Goal Shooter (GS) na Wing Attack (WA) kumepelekea timu yangu
kupoteza mchezo huu lakini naahidi kupata ushindi katika mechi ijayo dhidi ya
TTPL” alisema Nkurlu.
Naye,Kocha wa timu ya Ofisi
ya Rais (Utumishi) Bw. Mathew R. Kambona aliwapongeza wachezaji wake kwa
kuibuka na ushindi mnono na kuhaidi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza
katika mchezo huo ili kutengeneza mazingira mazuri ya kuendeleza wimbi la
ushindi katika mechi ijayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)