Vibrant

Friday, 2 May 2014

TIMU YA NETIBOLI YA UTUMISHI YAPONGEZWA KUNYAKUA UBINGWA MASHINDANO YA MEIMOSI 2014

Waziri wa Nchi-Utumishi Mh. Celina O. Kombani akiongea na wachezaji, pamoja na watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kuipongeza timu ya Utumishi kwa kutawazwa kuwa mabingwa katika Mpira wa Pete katika mashindano ya Mei Mosi 2014. iliyofanyika mapema leo. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Bw. HAB Mkwizu akimkaribisha mgeni rasmi  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (kushoto) kuongea na wachezaji wa ofisi yake na watumishi katika hafla fupi aliyoiandaa kuipongeza timu ya Utumishi kwa kuwa mabingwa wa Mpira wa Pete, Mei Mosi 2014 iliyofanyika ofisini kwake mapema leo 
Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (Mb), (hayupo pichani) katika hafla fupi ya kuipongeza timu ya Mpira wa Pete kwa kunyakua ubingwa kombe la Mei Mosi 2014 

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (Mb) akikabidhiwa kombe la ubingwa wa mpira wa Pete la Mei Mosi 2014 kutoka kwa Kapteni wa timu Elizabeth Fusi katika hafla fupi aliyoiandaa kuwapongeza mabingwa hao iliyofanyika ofisini kwake mapema leo
Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka mwenzao wa Ofisi ya Rais-Ikulu aliyepoteza maisha ghafla siku ya Mei Mosi 2014.