Mhe. Balozi Modest J. Mero, Balozi wa kudumu, Ubalozi wa Tanzania, Geneva akutana na Bi. Jan Beagle, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na UKIMWI (UNAIDS), katika ofisi ya ubalozi wa Tanzania tarehe hivi karibuni. Bi. Jan pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Bi. Jan alimtembelea Balozi kwa lengo la kumtaarifu juu ya majukumu ya bodi ya UNAIDS. Hii pia ni muendelezo wa mikutano ambayo Mhe Balozi anafanya na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu hapa Gevena, Uswisi.
Tanzania itakuwa moja wa wajumbe 22 wa bodi ya UNAIDS kwa mwaka huu 2014 kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2016. Katika mazungumzo, umuhimu wa kuendelea kuipa kipaumble mikakati ya kuzuia maambukizo mapya ya UKIMWI yalijadiliwa. Msimamo wa Tanzania katika kupambana na janga hili la UKIMWI uliwekwa bayana. Bi Jan alisifu juhudi za Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania katika kukabiliana na janga hili, ikiwa ni pamoja na juhudi za serikali inazo fanya kuchangia gharama kwa kuwa na mpango wa kuanzisha mfuko wa fedha wa kupambana na UKIMWI- AIDS Trust Fund(ATF). Mhe Balozi alimhakikishia Bi. Jan kwamba, Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha katika ushiriki wake kwenye bodi ya UNAIDS.
Modest Mero,Ambassador & Permanent Representative,
Permanent Mission of UR Tanzania
47 avenue Blanc,
1202 Geneva, Switzerland
Tel. +41 22 731 89 20
Fax: +41 22 732 82 55
Skype:mjmero2; tweeter: @mjmero