Vibrant

Wednesday, 2 April 2014

Tahadhari kwa wananchi!!!!!

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inawatahadharisha wananchi wote, ndani na nje ya nchi kujihadhari na watu wanaotumia jina la Utumishi kuwaibia fedha na kupoteza muda wao kufuatilia jambo ambalo halipo.
Watu hao wanatumia majina yafuatayo katika mitandao;
 Saving Foundation Loans na Jakaya Foundation kwa anuani http://savingfoundation.wapka.mobi/index.xhtml na kuelekeza kuwa Makao  Makuu yapo kwenye jengo la UTUMISHI.
Namba za simu zifuatazo zimekuwa zikitumika kuwatapeli wananchi watume fedha; 0715-373307, 0656-037520 na 0762-269376.
Wananchi epukeni kurubuniwa na watu hao kwani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma haijishughulishi na kutoa mikopo ya aina yoyote kwa wananchi.
Tangazo limetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
2 Aprili, 2014

Mawasiliano:  permsec@utumishi.go.tz, S.L.P 2483 Dar es Salaam,Simu: + (255) 22 2118531-4

No comments: