Vibrant

Wednesday 12 August 2015

Mwili wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Boniphace Haule aliyefariki nchini India wawasili jijini Dar es Salaam

Mwili wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Boniphace O. Haule ukiwa katika gari baada ya kupokelewa katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mwalimu J.K Nyerere.

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma waliofika kuupokea Mwili wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Boniphace O. Haule ulipowasili katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mwalimu J.K Nyerere.

TANZIA





Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Boniphace Haule - Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Pichani) kilichotokea nchini India tarehe 10.08.2015.
Mwili wa Marehemu utawasili leo, uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere. Mazishi yatafanyika Ijumaa tarehe 14/08/2015. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tegeta Ununio, Mtaa wa Mwaitende.

Maziko yanatarajia kufanyika katika makaburi ya KINONDONI.

Taarifa na taratibu za msiba zitafuata.

Monday 13 July 2015

MKUTANO WA 12 WA WAKUU WA UTUMISHI WA UMMA WA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA WAANZA


Mmoja wa Wajumbe wa mkutano wa Wakuu wa Utumishi wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika kutoka Afrika Kusini Bi.Colette Clark akipokewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni  Y. Sefue katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.

Taswira ya moja ya eneo mkutano wa Wakuu wa Utumishi Barani Afrika utakapofanyika.


Mmoja wa Wajumbe wa mkutano wa Wakuu wa Utumishi wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika kutoka Sierra Leone Bw. Ernest Surrur (kushoto) akipokewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni  Y. Sefue katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.


Mmoja wa Wajumbe wa mkutano wa Wakuu wa Utumishi wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika kutoka Rwanda Bw. Gaspard Musonera akipokewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni  Y. Sefue katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo.

Sunday 12 July 2015

MKUTANO WA 12 WA WAKUU WA UTUMISHI WA UMMA WA NCHI ZA AFRIKA WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA KUFUNGULIWA LEO na Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue akiongoza kikao cha maandalizi ya Mkutano wa  kumi na mbili (12) wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa nchi za Afrika Wanachama wa Jumuiya ya Madola  utakaofunguliwa leo.

 Katibu Wakuu na watendaji mbalimbali wakijadili wakati wa kikao: kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu . Dkt. Florens Turuka, akifuatiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimneti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhem James Meru.

 Taswira ya moja ya eneo mkutano wa Wakuu wa Utumishi Barani Afrika utakapofanyika.

Thursday 11 June 2015

6th Annual UNPAN Workshop in Johannesburg,South Africa

Executive Director of  the Center for Public Service Innovation (CPSI) Ms. Thuli Radebe giving welcoming remarks during the opening of 6th Annual Workshop held in Johannesburg, South Africa.

Session  in progress with delegates listening to UNDP Director for South Africa Mr. Walid Badawi.

Executive Director of the Center for Public Service Innovation (CPSI) Ms. Thuli Radebe offer a gift  to UNDP Director for South Africa Mr. Walid Badawi.


CPSI Programme Director   Mr. Pierre Choonraad moderate the event during day one at Emperors palace in Johannesburg. 


Friday 29 May 2015

UMOJA WA WATANZANIA WALIOSOMA NCHINI AUSTRALIA WAZINDULIWA RASMI

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (aliyesimama) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo. 

Waziri wa Afya na Utalii wa Australia Mh. Dkt. Kim Hames akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo.



Rais wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Watanzania  waliosoma nchini Australia wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Watanzania  waliosoma nchini Australia wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza na waandishi  habari baada ya kuzindua Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo  jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (aliyesimama) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza na Watanzania walionufaika na ufadhili wa masomo nchini Australia.

Tuesday 26 May 2015

SERIKALI YAMKARIBISHA NCHINI MWAKILISHI MKAZI MPYA WA JICA

Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kushoto) na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kulia) wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga  Bw. Tomonari Shinya iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo .

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kulia) na aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (wa pili kutoka kulia) katika hafla fupi ya kumuaga Bw. Shinya iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.Wengine ni Afisa Tawala Msaidizi wa JICA Bw. Nasibu Hamisi (wa tatu kutoka kulia) na Afisa Tawala  wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi. Mwanamridu Jumaa (wa nne kutoka kulia).

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi (kushoto) alipoitembelea Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akipeana kadi za mawasiliano na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. Katikati ni Mwakilishi Mkazi Mwandamizi mpya wa JICA nchini Bw. Takizawa Koichi akishuhudia.

Kaimu katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akimkabidhi zawadi Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA nchini aliyemaliza muda wake Bw. Tomonari Shinya (kulia) katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

Thursday 14 May 2015

HAZINA YAFANYA WARSHA KUHUSU MABORESHO YA FEDHA ZA UMMA


Msemaji wa Wizara ya Fedha, Bi. Ingiahedi Mduma akifafanua jambo wakati wa warsha ya siku tano kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma iliyofanyika katika Hoteli Njuweni Kibaha.
Washiriki wa warsha kuhusu maboresho ya matumizi ya fedha za umma iliyofanyika katika Hoteli ya Njuweni Kibaha


Washiriki wa warsha kuhusu maboresho ya matumizi ya fedha za umma iliyofanyika katika Hoteli ya Njuweni Kibaha
Bloggers wakiwa katika warsha kuhusu maboresho ya matumizi ya fedha za umma iliyofanyika katika Hoteli ya Njuweni Kibaha


Tuesday 5 May 2015

UTUMISHI YAFANYA MKUTANO MAALUM WA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Kaimu Katibu Mkuu - Utumishi Bw.HAB Mkwizu (aliyesimama)  akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika ukumbi wa hoteli ya J.B Belmonte mapema leo. Kulia kwake ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Lilian Denis.
Kaimu Katibu Mkuu - Utumishi Bw.HAB Mkwizu (aliyesimama)  akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma uliofanyika hoteli ya J.B Belmonte mapema leo. Wengine ni wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Utumishi.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa katika mkutano maalum wa Baraza la wafanyakazi uliofanyika hoteli ya J.B Belmonte mapema leo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (aliyesimama) akichangia mada katika mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma uliofanyika hoteli ya J.B Belmonte mapema leo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi wakifuatilia mada katika mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika hoteli ya J.B Belmonte mapema leo.

Tuesday 28 April 2015

Applications are hereby invited from qualified and experienced Tanzanians for the following vacant post advertised by the Southern African Development Community (SADC) Secretariat:

       THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE
PUBLIC SERVICE MANAGEMENT


VACANCY ANNOUNCEMENT

          Applications are hereby invited from qualified and experienced Tanzanians for the following vacant post advertised by the Southern African Development Community (SADC) Secretariat:-       

(i)           Senior Program Officer-Meteorology                                     
(ii)          Senior Program Officer-TBT
(iii)        Senior Finance Officer-FAT
(iv)        Senior Records and Archives Management Officer
(v)         Senior Program Officer –HIV/AIDS
(vi)        Senior Program Officer-Natural Resources and Wildlife
(vii)      Senior Officer –Agricultural Information
(viii)     Senior Officer-Politics and Diplomacy
(ix)        Legal Counsel
(x)         Librarian(Library, Records and Archives)
(xi)        Human Resources Officer Pay roll and Benefits
(xii)      IT Internal Auditor .
               
(i)   Deadline for Applications:   1th May, 2015                                                    
SUBMISSION OF APPLICATIONS:

n  For more information regarding Terms of Reference of the advertised post, qualifications, tenure of appointment, and remuneration please visit the Southern African Development Community website: (www.sadc.int) or see Annex I below.

n  All applicants should send two copies of  applications to:-

Permanent Secretary,
President’s Office,
Public Service Management,
Human Resources Development Division,
P.O. Box 2483,
DAR ES SALAAM.
Fax No: 2125299

Wednesday 1 April 2015

VACANCY ANNOUNCEMENT-East African Community (EAC) Secretariat

 

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE
PUBLIC SERVICE MANAGEMENT



Applications are hereby invited from qualified and experienced Tanzanians for the following vacant post advertised by the East African Community (EAC) Secretariat:
 (i)           Executive Secretary              (1 Post)
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(ii)          Deputy Executive Secretary (1 Post) 
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(iii)        Principal Heath Officer  -      (Clinical Research) (1 Post)       
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(iv)        Principal Heath Officer  -      (Operation and Applied Research)
(1 Post)      
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(v)         Accountant                             (1 Post)
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(vi)        Office Secretary/Administrative Assistant (1 Post)
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(vii)      Driver                                       (1 Post)
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(viii)     Court Recorder/ Transcriber (1 Post)
(i)   Duty Station:                        Arusha
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(ix)        Police Liaison Officer            (1 Post)
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(x)         Principal Civil Aviation Officer (1 Post)       
(i)   Duty Station:                        Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(xi)        Principal Accountant                     (1 Post)
(i)   Duty Station:                        East African Community-
Secretariet, Arusha Tanzania           
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(xii)      Senior Trade Officer (Competition) (1 Post)        
(i)   Duty Station:                       Bujumbura, Burundi
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

(xiii)     Protocol/Conference Officer (1 Post)
(i)   Duty Station:                        East African Community-
   Secretariet, Arusha Tanzania
(ii)  Deadline for Applications:   6th April, 2015

SUBMISSION OF APPLICATIONS:
 For more information regarding Terms of Reference of the advertised post, qualifications, tenure of appointment, and remuneration please visit the East African Community website: (www.eac.int)




Thursday 26 March 2015

KATIBU MKUU UTUMISHI ASTAAFU UTUMISHI WA UMMA

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akikabidhi ofisi kwa Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu baada ya kustaafu Utumishi wa Umma.Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwake leo.   

Wednesday 18 March 2015

MH.DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUMBUKUMBU DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu Dodoma leo.

Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, viongozi wa Serikali na Washirika wa Maendeleo kwa pamoja wakikata utepe kuzindua Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya faili lenye kumbukumbu za zamani katika Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu Dodoma leo.
HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE,
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KATIKA SHEREHE YA UFUNGUZI RASMI WA KITUO
 CHA TAIFA CHA KUMBUKUMBU
DODOMA TAREHE 18 MACHI, 2015

·        Waheshimiwa Mawaziri,
·        Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
·        Waheshimiwa Wabunge,
·        Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa,
·        Ndugu Makatibu Wakuu,
·        Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kumbukumbu
na Nyaraka za Taifa,
·        Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya
Mfuko wa Kuwaenzi Waasisi wa Taifa letu,
·        Ndugu Viongozi wa Taasisi Mbalimbali za Serikali,
·        Ndugu Wanahabari,
·        Wageni Waalikwa,
·        Mabibi na Mabwana.

Awali ya yote naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa kupata  nafasi ya kualikwa ili kuja kushirikiana nanyi katika tukio hili muhimu la ufunguzi rasmi wa   Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu  (The National Record Centre) hapa Dodoma. Kipekee napenda kuipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kuandaa shughuli hii. Pia ninawashukuru wageni wote kwa kuja kushiriki katika tukio hili muhimu.

Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana, Ninaamini mtakubaliana nami kwamba, kumbukumbu ni nyenzo muhimu katika utendaji kazi Serikalini na Taasisi zake. Bila ya kuwa na kumbukumbu sahihi hatuwezi kujua tunakotoka na tunakokwenda na hivyo kushindwa kufikia maamuzi sahihi kwa wakati. Kumbukumbu hutumika kama kielelezo katika uwajibikaji na ni nguzo muhimu katika Utawala Bora. Ili Serikali iweze kufikia lengo hilo na kuwezesha umma kujua mwenendo wa Serikali yao, lazima kuwe na kumbukumbu zinazotunzwa vizuri na zinazopatikana kwa urahisi. Kukosekana kwa taarifa sahihi na kwa wakati unaofaa kunaweza kuwafanya Watendaji wa Serikali kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa maamuzi au kutolewa kwa maamuzi yasiyo sahihi na yasiyokidhi matarajio ya wananchi. Aidha, ukosefu wa kumbukumbu hutoa mianya ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka na hata kuchelewesha au kuzuia haki kutendeka. Kasoro hizi huchangia sana katika kuzorotesha maendeleo ya uchumi wa Taifa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu Serikali yao na Taasisi zake.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, Programu ya Mabadiliko katika Utumishi wa Umma awamu ya pili (Public Service Reform Programme II – PSRP II) niliyoizindua mwezi Januari 2008, pamoja na mambo mengine ilijielekeza katika  kufanya mabadiliko kwenye mifumo ya utunzaji wa kumbukumbu na utoaji wa taarifa katika Utumishi wa Umma. Lengo kubwa la mabadiliko haya likiwa ni kuwa na Serikali yenye kuwajibika, uwazi na utawala bora. Chini ya Programu hii, Serikali iliona umuhimu wa kuangalia upya jinsi inavyozalisha taarifa zake, kuzitumia, kuzitunza na kuzihifadhi kwa ajili ya matumizi ya sasa na ya baadaye. Aidha, kabla ya uzinduzi wa Programu hii, Serikali ilibaini kuwepo kwa tatizo kubwa la utunzaji wa kumbukumbu hasa mlundikano mkubwa wa majalada katika Ofisi za Umma, ambayo yalihifadhiwa bila ya kufuata taratibu za utunzaji kumbukumbu. Hali hii kwa kiasi kikubwa pamoja na mambo mengine iliathiri utendaji wa Serikali katika kuwahudumia wananchi kama vile  ucheleweshaji wa kulipwa pensheni kwa watumishi wa umma, ugawaji holela wa viwanja na ucheleweshaji wa kusikilizwa kesi, rushwa na upotevu wa mali za umma. Kumbukumbu zinazotunzwa vizuri ni sawa na uti wa mgongo wa Serikali katika kufikia malengo yake kwa ukamilifu katika kutunga na kutekeleza Sera sahihi, kuweka mipango madhubuti, kuongeza ufanisi, tija, uwazi na uwajibikaji.


Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala cha CCM ya mwaka 2010, inasisitiza upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wananchi ambao ndiyo mamlaka iliyoiweka Serikali ya Awamu ya Nne madarakani. Aidha, Sera ya Taifa ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ya Mwaka  2010 na Sheria ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Na. 3 ya Mwaka 2002 zinaelekeza Serikali na Taasisi zake kuwa na majengo na vifaa vinayokidhi uhifadhi bora wa Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa. Kituo hiki ni moja ya vielelezo vya juhudi za Serikali katika kuhifadhi na kutunza kumbukumbu na nyaraka za Taifa ambazo ni dira ya kizazi kilichopo na kijacho kama sehemu ya urithi andishi na historia ya Taifa letu. Kuwepo kwa Kituo hiki, kutaongeza ufanisi katika utendaji na utoaji huduma bora kwa wananchi kwani kitakuwa ni chimbuko la taarifa mbalimbali zitakazoisaidia Serikali katika uendeshaji wa kazi zake za kila siku. 

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, Miundombinu ya Kituo hiki ni ya Kisasa na itakuwa na uwezo wa kuhifadhi majalada zaidi 770,000. Kutokana na uwezo wa Kituo kuhifadhi majalada hayo, Taasisi za Umma zitaokoa zaidi ya mita za mraba 77,700 za ofisi zao ambazo zilikuwa zikitumika kuhifadhi majalada haya. Aidha, miundombinu hii imezingatia uzalishaji wa taarifa za Serikali katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hivyo Kituo kimeunganishwa na mkongo wa Taifa ili kurahisisha mawasiliano Serikalini ikiwemo upatikanaji wa taarifa na nakala za kumbukumbu zitakazokuwa zinahitajika na watumiaji mbalimbali kwa haraka na uhakika zaidi kutoka katika Kituo hiki.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, Sera ya Taifa ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ya mwaka 2010 na Sheria ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Namba 3 ya mwaka 2002, zinaagiza Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kusimamia taratibu na mifumo ya utunzaji kumbukumbu, usalama wa kumbukumbu na nyaraka na kuwajengea uwezo watumishi wa masjala katika kutunza na kuwezesha Serikali kutoa huduma bora kwa raia wake. Napenda nichukue nafasi hii kuwakumbusha Watendaji Wakuu wa Ofisi mbalimbali za umma kuhusu wajibu wao wa kutunza kumbukumbu zinazozalishwa katika Ofisi zao kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali inayotolewa na mamlaka husika. Watendaji Wakuu wa Taasisi zote za Serikali wahakikishe wanahamishia katika Kituo hiki kumbukumbu zote zilizofungwa ili Kituo hiki kiweze kutunza kumbukumbu kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, Kazi iliyofanyika ya kusanifu, kujenga na kuweka vifaa vya kisasa vya kuhifadhia kumbukumbu ni nzuri na ya gharama kubwa. Nachukua nafasi hii, kuwaelekeza wote mnaosimamia uendeshaji wa Kituo hiki kuhakikisha kwamba kinatunzwa na kufanya kazi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.  Serikali kwa upande wake itaendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kutunza na kukiendeleza Kituo hiki ambacho ni cha pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana, Kabla sijamaliza hotuba yangu, naomba niwashukuru Washirika wetu  wa Maendeleo  kwenye Programu ya Mabadiliko katika Utumishi wa Umma, ambao kwa kushirikiana na Serikali yetu wamechangia katika kufanikisha ujenzi na uwekaji wa vifaa vya kisasa katika Kituo hiki.  Kwa kutambua umuhimu wa kumbukumbu na nyaraka walikubali kuchangia ujenzi wa Kituo hiki muhimu kwa nchi yetu. Hivyo, kwa namna ya pekee ninawashukuru sana Benki ya Dunia, Serikali ya Uingereza kupitia DfID na Serikali ya Canada kupitia CIDA kwa kuwezesha ujenzi wa Kituo hiki.

Mwisho ninapenda niwashukuru wote mliohudhuria sherehe hii ya ufunguzi wa Kituo cha Taifa cha Kumbukumbu - Dodoma.  Ni matarajio yangu kuwa Kituo hiki kitakuwa chachu ya kuleta uwajibikaji, uwazi na utawala bora kwa Taasisi zote za Serikali.


Asanteni kwa kunisikiliza!!