Vibrant

Sunday, 27 April 2014

JIPATIE KITENGE ORIGINAL KUTOKA CONGO!


Sale!Sale!Sale!
Vitenge vya Wax Original kabisa kutoka nchini Congo.
Bei ni nafuu.Vimebaki vichache wahi chako sasa.
Kama unahitaji wasiliana nami kwa namba hii 0717080903

UTUMISHI YAENDELEA KUTOA VICHAPO MASHINDANO YA MEI MOSI MOROGORO

Mchezaji wa Ofisi ya Rais, Utumishi Lilian Sylidion (GK) akinyaka mpira na kuwazidi wachezaji wa CDA Dodoma  katika mechi iliyochezwa jana ya mashindano ya Mei Mosi 2014 katika  Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mchezaji wa CDA ya Dodoma (mwenye mpira) akijianda kutoa pasi kwa huku akiwa kazingirwa na wachezaji wa Utumishi katika mechi iliyochezwa jana katika mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika  Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mwadawa Twalibu (GA) wa timu ya Ofisi ya Rais Utumishi akijiandaa kuchukua mpira licha ya upinzani wa wachezaji wa CDA Dodoma katika   mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika  Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mchezaji wa Ofisi ya Rais, Utumishi Sophia Komba  (C) akijiandaa kutoa pasi kwa Fatuma Machenga (GS) katika eneo la goli la wapinzani wao CDA Dodoma katika  mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika  Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Friday, 25 April 2014

Lets just fight! Kansiime Anne

UTUMISHI YAICHAKAZA CDA MASHINDANO YA MEI MOSI

Na. James Katubuka
Timu ya Mpira wa pete ya ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa bingwa wa michuano ya Mei Mosi mwaka huu mara baada ya kuilaza CDA ya Dodoma magoli 42 dhidi 15 katika mchezo uliofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani wa aina yake kutokana wachezaji wengi wa CDA kuwa ni wazoefu na Ofisi ya Rais Utumishi kuwa na wachezaji ambao wengi wao wameshaichezea timu ya Taifa kwa nyakati tofauti.

Licha ya washabiki wa mpira wa pete mjini Morogoro kushuhudia burudani safi pia walishuhudia jahazi la timu ya CDA likizama katika kipindi cha kwanza kwa kubugizwa  magori 16 dhidi ya matano katika mchezo huo.

Hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza kipenga cha mwisho kuashiria mchezo huo kwisha, wachezaji wa Ofisi ya Rais Utumishi Fatuma Machenga (GA) na Mwadawa Twalibu (GS) walishirikiana vema kuilaza CDA mabao 42 dhidi ya 15.

Nao wachezaji Anna Msulwa (WA) na Elizabeth Fusi (C) walikuwa ni chachu ya ushindi kwa timu ya utumishi kutokana na kuwalisha vema Fatuma Machenga (GA) na Mwadawa Twalibu (GS) katika mchezo huo uliotawiliwa na ufundi na shamla shamla toka timu pande zote mbili.

Mara baada ya mchezo kumalizika, kocha wa timu ya CDA Dodoma Bi. Susan Nkurlu alisema kuwa mchezo ulikuwa mzuri na wa kuvutia hivyo aliwapongeza wachezaji wake na wa Utumishi kwa kutoa burudani safi kwa wapenzi wa mpira wa pete wa Morogoro.

“Kukosekana kwa kwa wachezaji wangu nyota wawili Goal Shooter (GS) na Wing Attack (WA) kumepelekea timu yangu kupoteza mchezo huu lakini naahidi kupata ushindi katika mechi ijayo dhidi ya TTPL” alisema Nkurlu.

Naye,Kocha wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Bw. Mathew R. Kambona aliwapongeza wachezaji wake kwa kuibuka na ushindi mnono na kuhaidi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo huo ili kutengeneza mazingira mazuri ya kuendeleza wimbi la ushindi katika  mechi ijayo.






Wednesday, 23 April 2014

MEMBE KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA KIMATAIFA WA UALBINO

Na Frank Mvungi- Maelezo
WAZIRI wa wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi mkutano wa Kimataifa wa Ualbino utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Afisa Mahusiano na habari wa Chama cha Albino Tanzania (TAS),  Josephat Torner wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.

Torner alisema mkutano huo wa siku moja utafanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam na utawahusisha washiriki toka mataifa mbalimbali yakiwemo Nchi za Afrika Mashariki, Marekani, Nchi za Ulaya na Nchi za Kusini mwa Afrika.

Alisema moja ya matarajio ya mkutano huo ni kupata sauti ya pana ya Kimataifa kuutaka Umoja wa Mataifa kuitangaza tarehe 4 mwezi Mei kuwa Siku ya Kimataifa ya Ualbino.

Aliongeza kuwa lengo la maadhimisho ya siku hiyo ni kutafakari vikwazo vinavyosababisha tofauti ya umri wa kuishi kati ya watu wenye ulemavu na watu wengine.

“Hii inatokana na ukweli kwamba kwa Tanzania wastani wa umri wa kuishi kwa watu wenye ualibino ni miaka 30 wakati kwa watu wengine ni miaka 60”2, alisema Torner.

Alisema sababu zinazochangia watu wenye ulemavu wa ualbino kuishi nusu ya umri wa Watanzania wengine ni kukabiliwa na saratani ya ngozi.

Alitoa wito kwa watu wote wenye ualbino,wazazi,walezi na wadau mbalimbali na umma kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya.

Maadhimisho ya Siku ya Albino yalianzishwa hapa nchini mwaka 2006 na tangu mwaka huo yamekuwa  yakileta hamasa katika nchi mbalimbali Duniani.

Kilele cha maadhimisho hayo hapa nchini kinatarajiwa kuwa siku ya tarehe  4/5/2014 na kauli mbiu ikiwa ni Haki ya Afya,Haki ya Uhai.