Vibrant

Friday, 2 May 2014

TIMU YA NETIBOLI YA UTUMISHI YAPONGEZWA KUNYAKUA UBINGWA MASHINDANO YA MEIMOSI 2014

Waziri wa Nchi-Utumishi Mh. Celina O. Kombani akiongea na wachezaji, pamoja na watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kuipongeza timu ya Utumishi kwa kutawazwa kuwa mabingwa katika Mpira wa Pete katika mashindano ya Mei Mosi 2014. iliyofanyika mapema leo. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Bw. HAB Mkwizu akimkaribisha mgeni rasmi  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (kushoto) kuongea na wachezaji wa ofisi yake na watumishi katika hafla fupi aliyoiandaa kuipongeza timu ya Utumishi kwa kuwa mabingwa wa Mpira wa Pete, Mei Mosi 2014 iliyofanyika ofisini kwake mapema leo . 
Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (Mb), (hayupo pichani) katika hafla fupi ya kuipongeza timu ya Mpira wa Pete kwa kunyakua ubingwa kombe la Mei Mosi 2014 

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma  Mh. Celina O. Kombani (Mb) akikabidhiwa kombe la ubingwa wa mpira wa Pete la Mei Mosi 2014 kutoka kwa Kapteni wa timu Elizabeth Fusi katika hafla fupi aliyoiandaa kuwapongeza mabingwa hao iliyofanyika ofisini kwake mapema leo
Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka mwenzao wa Ofisi ya Rais-Ikulu aliyepoteza maisha ghafla siku ya Mei Mosi 2014.

Thursday, 1 May 2014

UTUMISHI YAKABIDHIWA KOMBE LA MSHINDI WA NETIBOLI MASHINDANO YA MEIMOSI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akikabidhi kombe kwa Kapteni wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi Bi. Elizabeth Fusi kwenye maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kombe hilo limekabidhiwa baada ya timu hiyo kuibuka  bingwa wa mchezo wa mpira wa pete katika mashindano ya Mei Mosi yaliyofanyika mjini Morogoro hivi karibuni.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utuimishi wa Umma wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Taifa kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utuimishi wa Umma wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Taifa kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utuimishi wa Umma (wenye bango) wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Taifa kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi.