Vibrant

Saturday, 8 March 2014

Siku ya Wanawake Duniani ilivyofana jijini Dar es Salaam

Waziri wa TAMISEMI Mh.Hawa Ghasia akihutubia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam Bw. Said Meck Sadiq akihutubia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam 
Kikundi cha burudani cha Machozi Theatre kikitoa burudan kwenye maadhimisho hayo.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Uhamiaji wakiwa kwenye maandamano
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa tayari kwa kuanza maandamano kuelekea viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam
Waziri wa TAMISEMI Mh.Hawa Ghasia (kushoto) akiserebuka wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Said Meck Sadick akimuunga mkono.
Baadhi ya washiriki kutoka ofisi mbalimbali za Serikali na binafsi wakitembelea mabanda kuangalia bidhaa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.

No comments: