Vibrant

Tuesday, 11 March 2014

MISA's Women to Watch in 2014:HOYCE TEMU

 
Hoyce is a communications specialist with the United Nations from Tanzania and has been chosen as one of MISA’s 2014 Women to Watch.   Every year, on 8 March, people all around the world celebrate International Women’s Day.  To commemorate the day in 2014, we are unveiling MISA’s Women to Watch – 12 women ... 
For more information follow the link below;

Taswira za Bunge la Katiba mjini Dodoma leo

Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba Bw.  Augustino Mrema akimweleza jambo Mjumbe mwenzie Bw. Islaim Aden Rage leo Mjini Dodoma.

Wajumbe wa Bunge Maalumla Katiba na Wajumbe wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu (Kulia) na Tundu Lissu wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.

Wajumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Hamadi Rashidi (kushoto) Juma Alawi (katikati) na Thumwein Thuwein wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Ally Kessy akiwaeleza jambo jambo Wajumbe wenzie Bw. Edward Lowassa (katikati) na Almas Maige ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta (kulia) akimweleza jambo Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.

Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu akiwaeleza jambo wajumbe wa bunge hilo wakati wa semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma. 
(PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO)

Monday, 10 March 2014

Matukio Bunge la Katiba leo Mjini Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Evod Mmanda bungeni Mjini Dodoma Leo.

Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Pandu Ameir Kificho akitoa maelekezo kwa wajumbe wa Bunge Hilo kabla ya Kuanza kwa Semina ya Uundaji wa kanuni zitakazoongoza bunge hilo, Mjini Dodoma Leo.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Wakisali Dua zilizoongozwa na Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo na Askofu Mstaafu Donald Mtetemela kabla ya Kuanza kwa Semina ya Uundaji wa kanuni zitakazoongoza bunge hilo, Mjini Dodoma Leo.

Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba na Mjumbe katika kamati ya kuunda kanuni zitakazzongoza Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu akijibu hoja iliyoulizwa na Moja ya Mjumbe wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma
 
(Picha na Hassan Silayo)

Saturday, 8 March 2014

Siku ya Wanawake Duniani ilivyofana jijini Dar es Salaam

Waziri wa TAMISEMI Mh.Hawa Ghasia akihutubia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam Bw. Said Meck Sadiq akihutubia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam 
Kikundi cha burudani cha Machozi Theatre kikitoa burudan kwenye maadhimisho hayo.

Baadhi ya watumishi wa Idara ya Uhamiaji wakiwa kwenye maandamano
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa tayari kwa kuanza maandamano kuelekea viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam
Waziri wa TAMISEMI Mh.Hawa Ghasia (kushoto) akiserebuka wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Said Meck Sadick akimuunga mkono.
Baadhi ya washiriki kutoka ofisi mbalimbali za Serikali na binafsi wakitembelea mabanda kuangalia bidhaa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Rais-Utumishi yampongeza Balozi Mteule Dkt. Aziz Mlima

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima iliyofanyika ukumbi wa Utumishi hivi karibuni.Kushoto kwake ni Balozi Mteule Dkt.Aziz Mlima na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Utumishi Bi.Jane Kajiru.

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akimkabidhi zawadi Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima katika hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika ukumbi wa Utumishi hivi karibuni. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Aziz Mlima alikuwa  Msaidizi wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Benjamin William Mkapa.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya RaisMenejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi Bw.George  Yambesi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Mteule Dkt. Aziz Mlima iliyofanyika ukumbi wa Utumishi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Balozi Mteule wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma baada ya hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika ofisini hapo hivi karibuni.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Utumishi Bw.George Yambesi na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu