Vibrant

Tuesday, 18 March 2014

OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA YAWAAGA WATAALAMU 6 WALIOMALIZA MUDA WA KUJITOLEA HAPA NCHINI

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (kulia) akitoa ufafanuzi wa maswali kutoka kwa waandishi wa habari baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japan iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Katibu Mkuu Utumishi Bw. George D. Yambesi akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzania Bw. Yasunori Onishi (kulia) akielezea kuhusu watalaam wa kujitolea kutoka nchini Japan  walivyofanya kazi hapa nchini katika hafla fupi ya kuwaaga wataalamu hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.


Mtaalamu wa Kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu  kutoka Japan Bw. Tomotaka Tani akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wake hapa nchini, katika hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita waliomaliza muda wao hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.

Mtaalamu wa Kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu  kutoka Japan Bw. Tomotaka Tani akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wake hapa nchini, katika hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita waliomaliza muda wao hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.


Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akitoa zawadi kwa Mtaalamu wa kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu kutoka Japan Bw.  Jun Tsuda (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita wa kujitolea kutoka nchini Japani iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzanian Bw. Yasunori Onishi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yambesi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini.Wengine ni baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Mtaalamu wa Kujitolea katika fani ya Sayansi na Hesabu  kutoka Japan Bw. Tomotaka Tani (kushoto) akijibu maswali ya Mwandishi wa Habari wa gazeti la  Daily News Bi. Hilda Mhagama baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalamu sita waliomaliza muda wao hapa nchini iliyofanyika ukumbi wa Utumishi mapema leo.

 

Sunday, 16 March 2014

MHE. BALOZI MODEST J MERO, AKUTANA NA BI. JAN BEAGLE, NAIBU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINANOPAMBANA NA UKIMWI (UNAIDS) AMBAYE PIA NI NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA




Mhe. Balozi Modest J. Mero, Balozi wa kudumu, Ubalozi wa Tanzania, Geneva akutana na Bi. Jan Beagle, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na UKIMWI (UNAIDS), katika ofisi ya ubalozi wa Tanzania tarehe hivi karibuni. Bi. Jan pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,




Bi. Jan alimtembelea Balozi kwa lengo la kumtaarifu juu ya majukumu ya bodi ya UNAIDS. Hii pia ni muendelezo wa mikutano ambayo Mhe Balozi anafanya na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu hapa Gevena, Uswisi.



Tanzania itakuwa moja wa wajumbe 22 wa bodi ya UNAIDS kwa mwaka huu 2014 kwa kipindi cha miaka mitatu hadi 2016. Katika mazungumzo, umuhimu wa kuendelea kuipa kipaumble mikakati ya kuzuia maambukizo mapya ya UKIMWI yalijadiliwa. Msimamo wa Tanzania katika kupambana na janga hili la UKIMWI uliwekwa bayana. Bi Jan alisifu juhudi za Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania katika kukabiliana na janga hili, ikiwa ni pamoja na juhudi za serikali inazo fanya kuchangia gharama kwa kuwa na mpango wa kuanzisha mfuko wa fedha wa kupambana na UKIMWI- AIDS Trust Fund(ATF). Mhe Balozi alimhakikishia Bi. Jan kwamba, Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha katika ushiriki wake kwenye bodi ya UNAIDS.
Modest Mero,

Ambassador & Permanent Representative,

Permanent Mission of UR Tanzania

47 avenue Blanc,

1202 Geneva, Switzerland

Tel. +41 22 731 89 20

Fax: +41 22 732 82 55

Skype:mjmero2; tweeter: @mjmero



Utumishi yafanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha mwaka


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR MUU), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa OR MUU Bw. George D. Yambesi, katikati, akiendesha mkutano wa Baraza la Wafanyakazi hivi karibuni, kulia ni Naibu Katibu Mkuu OR MUU Bw. HAB Mkwizu na kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bi. Lilian Dennis

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR MUU), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa OR MUU Bw. George D. Yambesi, kushoto, akisikiliza hoja zilizowasilishwa na Watumishi wa Ofisi yake katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni, kulia ni Naibu Katibu Mkuu OR MUU Bw. HAB Mkwizu.


Sehemu ya wajumbe wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza (hayupo pichani) wakati wamkutano hyuo uliofanyikla hivi karibuni.