Wednesday, 30 April 2014
MABADILIKO YA ANUANI YA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma inapenda kuwafahamisha wadau wake kuwa anuani yake
imebadilika hivyo kuanzia sasa mawasiliano yafanyike kwa kutumia anuani
ifuatayo;
OFISI
YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
UTUMISHI
HOUSE
8
BARABARA YA KIVUKONI
11404
DAR ES SALAAM
au
PRESIDENT’S
OFFICE, PUBLIC SERVICE MANAGEMENT
UTUMISHI
HOUSE
8
KIVUKONI ROAD
11404
DAR ES SALAAM
Anuani hii inachukua nafasi
ya Sanduku la Posta 2483, Dar es salaam. Hivyo, mawasiliano yote yazingatie
anuani mpya.
Limetolewa
na
Katibu
Mkuu
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Barua
pepe; permsec@utumishi.go.tz
Tuesday, 29 April 2014
UTUMISHI YATWAA UBINGWA MASHINDANO YA MEI MOSI 2014
| Wachezaji wa Ofisi ya Rais, Utumishi wakipasha misuli moto (warm-up) jana kabla ya mechi ya mashindano ya Mei Mosi 2014 dhidi ya Uchukuzi iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro |
Na.
James Katubuka
Ofisi ya Rais,Menejimenti ya
Utumishi wa Umma imeibuka kinara wa mpira wa pete katika mashindano ya Mei Mosi
ya mwaka huu yaliyofikia tamati jana katika kiwanja cha Jamhuri mjini Morogoro.
Utumishi walijikita kileleni
mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuisambaratisha timu ya Wizara ya Uchukuzi
kwa kuibugiza magoli 33 dhidi ya 21 katika mchezo uliokuwa na ushindani na
msisimko wa aina yake uliorindima katika Uwanja mkongwe wa Jamhuri Morogoro.
Mchezaji Fatuma Machenga
(GS) wa Ofisi ya Rais (Utumishi) alikuwa mwiba dhidi ya timu ya Uchukuzi kwa
kuiongoza Utumishi vema katika mchezo huo.
Aidha,Goal Shooter (GS) huyo
wa Utumishi ndiye mfungaji bora wa mashindano ya Mei Mosi kwa mpira wa pete
ambapo amefunga magoli 136 yaliyopelekea kunyakua kikombe cha ufungaji bora.
Akizungumzia hali ya mchezo
baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho, Mchezaji Subira Jumanne (WA) wa timu
ya Uchukuzi alisema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kwani walikutana na
timu nzuri na iliyojiandaa vema.
“Asiyekubali kushindwa si
mshindani hivyo tutafanya maandalizi ya kutosha ili katika mashindano yajayo nasi
tuwe mabingwa” alisema Subira.
Naye,mfungaji bora wa
mshindano hayo mchezaji Fatuma Machenga (GS) wa Utumishi akiwa mwenye furaha
alisema kuwa anajisikia fahari kuiwezesha timu yake kuwa bingwa.
“Tutahakikisha kuwa mwakani
tunapambana kwa hali na mali ili tuweze kutetea ubingwa wetu” alisema Machenga.
Utumishi imenyakua kombe
hilo lililokuwa likishikiliwa na timu ya Wizara ya Ulinzi ambao ndio walikuwa
mabingwa wa Mei Mosi 2013.Kikombe cha mshindi wa pili kwa mwaka huu kimenyakuliwa na Wizara ya
Mambo ya Ndani na mshindi wa tatu ni Wizara ya Uchukuzi.
Monday, 28 April 2014
VACANCY ANNOUNCEMENT-AFRICAN RISK CAPACITY
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT'S OFFICE
Applications are hereby
invited from qualified and experienced Tanzanians for the following Vacant post
advertised by the African Risk Capacity (ARC)
·
Post : Director General
·
Duty Station : Pretoria
- South Africa
·
Deadline for
Applications : 30th
April 2014
SUBMISSION OF
APPLICATIONS
For
more information regarding Terms of Reference of the advertised posts;
qualifications, tenure of appointment, and remuneration please visit the African Risk Capacity (ARC): http://www.africanriskcapacity.org/arcdg/application
·
All the applications
should be made through the online system only via the following website: erica.hovanibue@africanriskcapacity.org
·
Copy of the
applications should be sent to the following address:-
Permanent Secretary,
President’s Office-Public Service Management,
P.O. Box 2483,
DAR
ES SALAAM.
E-mail:
permsec@estabs.go.tz
Subscribe to:
Posts (Atom)
