Vibrant

Wednesday, 5 March 2014

Matukio katika picha Bunge la Katiba mjini Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akimweleza jambo Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Mohamed Seif Khatib (kulia) Wakati wa Kikao cha Semina uundwaji wa Kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila akitoa hoja yake wakati wa Kikao cha Semina uundwaji wa Kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Christopher Ole Sendeka akichangia mjadala kuhusu vifungu vya kanuni vitakavyotumika katika Bunge Maalum la Katiba.


Mweyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Pandu Ameir Kificho akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati inayoshughulikia uundwaji wa kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba Bi. Mgeni Juma akisoma baadhi ya vifungu vya kanuni vilivyofanyiwa marekebisho leo Mjini Dodoma.

Picha zote na Hassan Silayo (Habari-MAELEZO)

No comments: