Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimweleza jambo Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Jovina Bujulu leo Mjini Dodoma. |
Na Jovina Bujulu-Maelezo, Dodoma
Ubora wa elimu ya juu umeendelea kuimarika kwa kiasi
kikubwa kutokana na kuwepo kwa Taasisi za muungano kama Bodi ya Mikopo ya Elimu
ya Juu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano) Bi. Samia Suluhu Hassan wakati wa mahojiano na Afisa Habari wa
Idara ya Habari (MAELEZO) leo Mjini Dodoma.
Waziri Samia alisema kuwa kupitia Taasisi hizo wanafunzi
wenye sifa kutpoka Tanzania Bara na Zanzibar wanapatiwa Mikopo ili kukidhi
gharama za masomo.
“kumekuwepo na ushirikiano katika suala la elimu ya
juu kwa mfano kati ya wanafunzi 600 kutoka zanzibar wanaodahiliwa na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania,
400 kati yao wanapatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Tanzania
Bara na 200 waliosalia wanapatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya ndani ya Zanzibar
kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ” alisema Waziri Samia.
Akifafanua zaidi kuhusu umimarikaji wa Elimu ya Juu Waziri
Samia alisema kuwa, Mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na Chuo chochote cha Elimu ya
Juu lakini kutokana na msisitizo uliowekwa katika kuiwezesha sekta hiyo Zanzibar
imefanikiwa kuwa na vyuo vikuu 5.
Waziri Samia Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni State
University of Zanzibar (SUZA), Zanzibar University, Chuo cha Elimu cha Chukwani,
chuo cha Afya na Chuo cha Fedha.
Serikali zitaendelea kuhakikisha kwamba nchi
inaendelea kuwa yenye umoja, Amani , Utulivu na Usalama ili Muungano wetu
uendelee kudumu na kuimarika kwa faida yetu na Vizazi Vijavyo.
No comments:
Post a Comment