WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Na Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali imejipanga
kukamilisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja Mipakani (One Stop Border
Posts-OSBP) vitakavyosaidia kurahisisha taratibu za forodha,uhamiaji,Usimamizi
wa ubora wa bidhaa na huduma ,usalama na ulinzi kwa kutoa huduma hizi upande
mmoja wa mpaka.
Hayo yamesemwa
na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Vedastinian Jastinian wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza faida
za vituo hivyo, Vedastinian amesema vitaondoa urasimu uliokuwepo awali na
kuharakisha huduma na kwa wananchi wa nchi wanachama wakati wanapotaka
kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Alisema Kituo
cha kwanza ni kile cha Holili ambacho kimekamilika na kimekabidhiwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao
ndio waendeshaji wa vituo hivyo hapa nchini ambapo mradi huu unatarajiwa
kukamilika mwezi Mei 2014.
Alifafanua kuwa
katika mipaka ya Sirari/Isebania unazitenganisha Tanzania na Kenya na kwa
upande wa Mkoa wa Mara mpaka wa Mutukula unazitanganisha Tanzania na Uganda.
Vedastinian alivitaja
vituo vingine kuwa ni Namanga cha Arusha,Kabanga/Kobero kilichopo mpakani mwa
Tanzania na Burundi unatarajiwa kukamilika mapema mwezi novemba 2014.
Alitaja vituo
vingine ni Horohoro Mkoani Tanga na Lungalunga upande wa nchi ya Kenya ambapo
ujenzi wake unatarajia kukamilika mapema mwaka huu.
Mradi huo
unatekelezwa baada ya kutungwa sheria ya jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuanzisha
vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja mipakani (OSBP) Katika nchi wanachama wa
jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sheria
iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na Iko katika hatua za mwisho za
kuidhinishwa na Wakuu wan chi wanachama.
No comments:
Post a Comment