Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya
habari wakifuatilia mkutano wa Shirika la Viwango Tanzania uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
|
Na Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali imedhamiria
kuwainua wajasiriamali wadogo hapa nchini ili kuongeza uzalishaji wa Bidhaa za
ndani zitakazosaidia kuimarisha uchumi wa Taifa.
Hayo yamesemwa
na Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la viwango hapa nchini (TBS) Tumaini Mtitu wakati wa Mkutano na waandishi
wa Habari leo jijini Dar es salaam.
Alisema shirika
hilo limekuwa likishirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo (Sido) kuwajengea
uwezo wajasirimali wadogo ili hatimaye wazalishe bidhaa zenye ubora na hivyo kupata
cheti cha ubora kinachotolewa na shirika hilo.
Mtitu aliongeza
kuwa wajasiriamali wote wanaojihusisha na uzalishaji wa bidhaa hapa nchini
wanatakiwa kuthibitishwa na shirika hilo ili kuwalinda watumiaji wa bidhaa hizo
kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Aliwataka Wajasiriamali
hao kupitia SIDO ili waweze kujengewa uwezo wa kuzalisha bidhaa bora na baada
ya hapo bidhaa zao ziweze kukaguliwa na kama zikikidhi vigezo wapate cheti cha
ubora ambapo mchakato huo unaweza kuchukua mwezi mmoja.
Akizungumzia faida
za Wajasiriamali kupata cheti cha ubora baada ya bidhaa zao kukidhi vigezo
vilivyowekwa na shirikika hilo, Mtitu alisema unawawezesha wajasiriamali
kupanua wigo wa soko la bidhaa zao na kuwa
wa kimataifa.
Wakati huo huo Mtitu
aliwataka watanzania wote kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali kupitia
shirika hilo ili waweze kupata cheti cha ubora na kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Utaratibu wa
kupata alama ya ubora ni kwanza kuwasilisha maombi kwa mkurugenzi Mkuu wa TBS,
ukaguzi wa awali na upimaji wa Sampuli za bidhaa husika na hatimaye kutolewa
kwa cheti cha ubora baada ya bidhaa husika kukizi vigezo.
No comments:
Post a Comment