Vibrant

Wednesday, 16 April 2014

SERIKALI YASAINI MKATABA WA KUSIMIKA MTANDAO WA MAWASILIANO WA SERIKALI

Katibu Mkuu Utumishi Bw. George D. Yambesi (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa kuweka Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali  na kampuni za mawasiliano za SOFTNET Technologies na TTCL iliyofanyika ofisini kwake jana. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt Kuwe Bakari, kushoto ni Bw. Priscus Kiwango Mkurugenzi wa TEHAMA Utumishi, akifuatiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya SOFTNET Ltd  Bw.Gilbert Herman 

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akimkabidhi mkataba wa kuweka mtandao wa Mawasiliano wa Serikali Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt.Kuwe Bakari wakati wa hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake jana. 

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi akimkabidhi mkataba wa kuweka mtandao wa Mawasiliano wa Serikali Mkurugenzi wa kampuni ya  SOFTNET Technologies Ltd Bw. Gilbert Herman wakati wa hafla fupi ya kusainiana mkataba huo iliyofanyika Utumishi jana. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt.Kuwe Bakari. 

Katibu Mkuu Utumishi Bw. George D. Yambesi (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa kuweka Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali  na kampuni za mawasiliano za SOFTNET Technologies na TTCL iliyofanyika jana Ofisini kwake. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt Kuwe Bakari, kushoto ni Bw. Priscus Kiwango Mkurugenzi wa TEHAMA Utumishi, akifuatiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya SOFTNET Ltd  Bw.Gilbert Herman 

Baadhi ya wajumbe walioshiriki hafla fupi ya kusaini mkataba wa kuweka Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali  na kampuni za mawasiliano za SOFTNET Technologies na TTCL iliyofanyika jana Ofisini kwake.

Monday, 14 April 2014

TBS KUINUA WAJASIRIAMALI WADOGO NCHINI

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Vedastina Justinian akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mradi wa Vituo vya Utoaji Huduma kwa Pamoja Mipakani (One Stop Border Posts) unaolenga kurahisisha taratibu za forodha, uhamiaji, usimamizi wa ubora wa bidhaa, ulinzi na usalama. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi Mhandisi Abdillah Mataka na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.

Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi kutoka Wizara ya  Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhandisi Abdillah Mataka, akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo katika kujenga vituo vya utoaji huduma mipakani kwa kila nchi husika ili kurahisisha shughuli za utoaji huduma za forodha na uhamiaji. Ujenzi wa vituo hivyo hapa nchini unafadhiliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo ya Japan. Kushoto ni Mchumi Idara ya Biashara na Sekta za Uzalishaji kutoka wizara hiyo Bw. Amedeus Mzee.

Mchumi Idara ya Biashara na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Amedeus Mzee akizungumzia faida zitakazopatikana kwenye mradi wa vituo vya utoaji huduma kwa pamoja mipakani, aidha alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na watumishi wa vituo hivyo katika kuhakikisha mapato hayapotei kwa maslahi ya nchi yetu na jumuiya kwa ujumla.

SERIKALI KUKAMILISHA VITUO VYA UTOAJI HUDUMA MIPAKANI

WIZARA YA  USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Na Frank Mvungi-Maelezo

Serikali imejipanga kukamilisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja Mipakani (One Stop Border Posts-OSBP) vitakavyosaidia kurahisisha taratibu za forodha,uhamiaji,Usimamizi wa ubora wa bidhaa na huduma ,usalama na ulinzi kwa kutoa huduma hizi upande mmoja wa mpaka.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vedastinian Jastinian wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akieleza faida za vituo hivyo, Vedastinian amesema vitaondoa urasimu uliokuwepo awali na kuharakisha huduma na kwa wananchi wa nchi wanachama wakati wanapotaka kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Alisema Kituo cha kwanza ni kile cha Holili ambacho kimekamilika na kimekabidhiwa  kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao ndio waendeshaji wa vituo hivyo hapa nchini ambapo mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2014.
Alifafanua kuwa katika mipaka ya Sirari/Isebania unazitenganisha Tanzania na Kenya na kwa upande wa Mkoa wa Mara mpaka wa Mutukula unazitanganisha Tanzania na Uganda.

Vedastinian alivitaja vituo vingine kuwa ni Namanga cha Arusha,Kabanga/Kobero kilichopo mpakani mwa Tanzania na Burundi unatarajiwa kukamilika mapema mwezi novemba 2014.

Alitaja vituo vingine ni Horohoro Mkoani Tanga na Lungalunga upande wa nchi ya Kenya ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika mapema mwaka huu.
Mradi huo unatekelezwa baada ya kutungwa sheria ya jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuanzisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja mipakani (OSBP) Katika nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sheria iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na Iko katika hatua za mwisho za kuidhinishwa na Wakuu wan chi wanachama.