Vibrant

Wednesday, 26 March 2014

WAJUMBE BUNGE LA KATIBA WATAKIWA KUZINGATIA MASLAHI YA TAIFA

Na  Magreth  Kinabo – Maelezo, Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Maalum la Katiba wamewataka wajumbe wenzao kujitika katika mchakato wa mjadala wa Rasimu ya Katiba Mpya  itakayozingatia maslahi ya taifa na kuwanufaisha Watanzania badala kujitazama mwenyewe.

Kauli hiyo imetolewa leo na mjumbe wa bunge hilo, ambaye ni mmoja wa kiongozi wa kundi la TANZANIA KWANZA Dk. Emmanuel Nchimbi  wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo  kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la  Tanzania(TBC), ambapo alisema msingi wa kundi hilo ni kushiriki katika mchakato huo  na kuaichaTanzania ikiwa moja.
“ Tunataka kushiriki katika kumaliza kazi ya  Bunge hili na kuaicha Tanzania ya leo na Kesho baada kumaliza ,” alisema Dk. Nchimbi.

 Aidha DK . Nchimbi alisema  kuwa mchakato huo usiwe sehemu ya kujipatia madaraka, bali iwe ya kuwaongoza Watanzania katika kuwapatia maendeleo.
Alisema bado watu wana mahitaji makubwa ya huduma za kijamii kama vile  elimu, afya, ufugaji, na miundombinu.

Dk. Nchimbi akifafanua kuhusu suala la kura ya wazi au siri, alisema bado msimamo wake  ni wa kura ya wazi  ambao utajenga mfumo wa maadili ya ukweli na uwazi, huku akihoji kama wanachangia mjadala kwa wazi kwa nini kura zisipigwe kwa wazi?
Alisema kura ya wazi itasaidia wananchi kutambua michango yao katika maeneo mbalimbali ilivyowakilishwa.

 “Tuko hapa kutunga Katiba ya Watanzania mtu atakumbukwa kwa kile alichokisema,” alisisitiza.

Kwa upande wake mjumbe mwingine wa  kundi hilo , Charles Mwijage akingumza katika kipindi hicho aliwataka wajumbe wa Bunge hilo kutumia njia ya maridhiano pale wanapoona kuna mambo ambayo hajaridhika nayo.

 Akizungumzia kuhusu suala la kuwepo kwa Serikali tatu alisema , lina gharama ya kuuendeshaji kwani ,italazimika kuwa na tume nane kuwa na mabunge matatu yenye viongozi tofauti ambayo yataongeza gharama

 Akizungumza baada ya kuahirishwa wa kikao cha  Bunge hilo, mjumbe kutoka Asasi ya Vijana, Siti Abbas Ali , ambaye pia ni Mwanasheria kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) aliwataka Watanzania kuondoa hofu juu ya  mchakato huo,hivyo katiba hiyo itakuwa ni ya Watanzania.

 Alisema wataangalia kwa upana haki za vijana, watoto, wanawake na makundi maalum kwa upana. Mwisho.

No comments: