Vibrant

Saturday, 8 March 2014

Ofisi ya Rais-Utumishi yampongeza Balozi Mteule Dkt. Aziz Mlima

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima iliyofanyika ukumbi wa Utumishi hivi karibuni.Kushoto kwake ni Balozi Mteule Dkt.Aziz Mlima na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Utumishi Bi.Jane Kajiru.

Katibu Mkuu Utumishi Bw.George D. Yambesi (kushoto) akimkabidhi zawadi Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima katika hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika ukumbi wa Utumishi hivi karibuni. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Aziz Mlima alikuwa  Msaidizi wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Benjamin William Mkapa.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya RaisMenejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Utumishi Bw.George  Yambesi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Mteule Dkt. Aziz Mlima iliyofanyika ukumbi wa Utumishi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Balozi Mteule wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma baada ya hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika ofisini hapo hivi karibuni.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Utumishi Bw.George Yambesi na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu

Thursday, 6 March 2014

Wanafunzi watakiwa kuchukua hatua wanapokutana na aina yeyote ya udhalilishaji wa kijinsia.

Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Tarehe 8, Machi kila mwaka, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari leo Mjini Dodoma. Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Jovina Bujulu

Matukio Bunge Maalum la Katiba Dodoma leo

Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (Kushoto) akimweleza jambo mjumbe mwenzie Bw. Saleh Pamba baada ya Bunge hilo kuahirishwa, leo Mjini Dodoma

Wednesday, 5 March 2014

Muungano wa Tanzania waendelea kuimarisha ubora wa Elimu ya Juu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimweleza jambo Afisa Habari Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Jovina Bujulu leo Mjini Dodoma.
Na Jovina Bujulu-Maelezo, Dodoma
Ubora wa elimu ya juu umeendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwepo kwa Taasisi za muungano kama Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bi. Samia Suluhu Hassan wakati wa mahojiano na Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Mjini Dodoma.
Waziri Samia alisema kuwa kupitia Taasisi hizo wanafunzi wenye sifa kutpoka Tanzania Bara na Zanzibar wanapatiwa Mikopo ili kukidhi gharama za masomo.
“kumekuwepo na ushirikiano katika suala la elimu ya juu kwa mfano kati ya wanafunzi 600 kutoka zanzibar  wanaodahiliwa na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania, 400 kati yao wanapatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Tanzania Bara na 200 waliosalia wanapatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya ndani ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ” alisema Waziri Samia.
Akifafanua zaidi kuhusu umimarikaji wa Elimu ya Juu Waziri Samia alisema kuwa, Mwaka 1964, Zanzibar haikuwa na Chuo chochote cha Elimu ya Juu lakini kutokana na msisitizo uliowekwa katika kuiwezesha sekta hiyo Zanzibar imefanikiwa kuwa na vyuo vikuu 5.
Waziri Samia Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni State University of Zanzibar (SUZA), Zanzibar University, Chuo cha Elimu cha Chukwani, chuo cha Afya na Chuo cha Fedha.
Serikali zitaendelea kuhakikisha kwamba nchi inaendelea kuwa yenye umoja, Amani , Utulivu na Usalama ili Muungano wetu uendelee kudumu na kuimarika kwa faida yetu na Vizazi Vijavyo.
 

Matukio katika picha Bunge la Katiba mjini Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akimweleza jambo Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Mohamed Seif Khatib (kulia) Wakati wa Kikao cha Semina uundwaji wa Kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi